Let Love Lead

Friday, September 14, 2018

FAHAMU : MAMBO YA MSINGI YATAKAYOFANYA UPENDO WAKO USTAWI VIZURI


Upendo wa kweli katika mahusiano ya kimapenzi ni lazima kuwe na vitu ambavyo viataonyesha upendo huo ukue kila wakati, miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na:

1. Upendo unahitaji upole.
upendo hauwezi kudumu katika ukali upendo unajengwa na upole maana upole hujenga bali hasira ubomoa upendo,uwe mpole unapozungumza na mwenzi wako upole hugeuza hugeuza hasira hasara.

Hivyo ili ufanikiwe katika kutunza mahusiano yenu unatakiwa uwe mpole hata kama umesika kitu kibaya kwa mwenzi wako unatakiwa uwe mpole ili uweze kufanikiwa kujua unachotaka kujua Upole ni mlezi wa upendo.

2. Kutetea (Defending) .
Upendo unahitaji utetezi, Unajua unavyoamua kumpenda mtu unatakiwa umtetee unapoona ananenewa mabaya usichangie kunena mabaya juu ya mapenzi wako usimchafue mpenzi wako, hatua uliyofanya kumpenda tayari umefanyika mtetezi wa mpenzi wako, usikubari dada, mama, baba, mjomba,na marafiki zako wanamnena mabaya mpenzi wako mtotoe kwa bidii ficha aibu ya mwenzi wako .

Ukitaka Upendo usiharibike na uimalike unatakiwa uwe mtetezi mzuri kwa mwenzi wako. Hivyo upendo unahitaji mtetezi.

3.  Kutoshelezwa (satisfication)
Upendo unahitaji kutosheleza upendo hauhitaji kulipuriwa unahitaji utoshelezwe unatakiwa kumtosheleza mwenzi wako sawa usiwe kama kuku upendo hauhitaji kilipuliwa unahitaji kutoshelezwa.

4. Furahi (Enjoyment)
Upendo unahitaji furaha unatakiwa umfurahishe mpenzi wako kwa kila kitu mfanye afulahi na kufurahia upendo wako unaompa.

5. Hisia (Fellings)
Upendo unahitaji hisia unatakiwa kuonyesha hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako unajua kuwa upendo ni hisia kali. Muoneshe mpenzi wako hisia kali za mapenzi ulizonazo kwake maana upendo ili ukuwe unahitaji mtu mwenye hisia za mapenzi.