Let Love Lead

Thursday, September 20, 2018

FAHAMU : NGUVU YA KUJITAMBUA UKIWA BADO KIJANA


JENGA UFAHAMU
Kujitambua ni hatua ya muhimu katika maisha ya mtu yoyote duniani na ni hatua ambayo hakuna mwanadamu anaeweza kufika hatima ya maisha yake kwa ubora na matarajio bila kuipita. Kujitambua ni matokeo ya kupata ufahamu sahihi juu eneo Fulani, ingawa pia inawezekana mtu akajitambua kwa kupata ufahamu usio sahihi utakaomfanya aishi maisha yanayolingana na ufahamu alioupata. Ufahamu unapatikana kwa kutafuta, kuchunguza na kudadisi taarifa mbalimbali lugha rahisi ufahamu ni gharama. Matokeo ya ufahamu ulionao yatafanana na ubora wa maisha unayoishi. Kila taarifa unayoipata ina kusudi au lengo lake, uwe unajua au hujui na ni muhimu kuzingatia kuwa kiwango cha matokeo ya kujitambua kitafanana na ubora wa taarifa ulizozipata. Udhihirisho wa maisha ya kujitambau ni hatua ya juu kabisa ya kuthibitisha kwamba kweli umejitambua.
*Maana ya Kujitambua

“Kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na nguvu ya taarifa unazopata”

Umuhimu wa kujitambua ukiwa bado kijana, nguvu ya kujitambua ukiwa bado kijana, thamani ya kujitambua ukiwa bado kijana na kusudi la kujitambua ukiwa bado kijana ni:

*Udhihirisho wa ubora wa maamuzi yako,

*Udhihirisho wa ubora wa maisha yako

*Kusimamia maamuzi na matokeo yake bila kutoa visingizio

*Matokeo yanayoonekana kuathiri maisha yako

*Ufahamu unaojitosheleza katika kufanya chaguzi mbali mbali za maisha kwa kuzingatia nafasi ya Mungu kwako

*Kuishi maisha yanayoongozwa na kanuni za Ufalme wa Mungu

*Uwezo wa kuishi na watu wenye tabia na mwenendo tofauti bila kuathiri kanuni za maisha yako kiMungu
JIULIZE..

*Je! Maisha yangu yanawasaidia wengine kupata tumaini katika wito walioitiwa?

*Je! Ni kitu gani kinachonizuia nisiishi sawa na mpango wa Mungu?

*Je ninamruhusu Mungu kunitumia au namzuia kunitumia kwa jinsi nilivyo?

*Je nina muda wa kutosha kuutafakari, kuuombea na kuupanga wakati wa maisha yangu ya baadae?

*Mungu anataka nini kwenye maisha yangu kwa ujumla wake?

*Je maisha yangu yana mchango wowote katika jamii katika kuujenga ufalme wa Mungu.

*Je! ninafanyika Baraka mbele za Mungu na watu wanaonizunguka kwa mwenendo wangu?

*Ni kitu gani kinaniongoza kwenye maisha yangu kufanya yote ninayoyafanya kila siku?
*Wewe ni nani?

*Kitu gani kinakutambulisha katika ulimwengu wako na wengine?

*Kwanini umeumbwa kwa upekee ulionao?

*Nini kusudi la kuwepo kwako duniani, kwenye familia yako, Tanzania?

*Nafasi yako ni ipi kwako binafsi, familia, jamii, kanisa, taifa na Ufalme wa Mungu?

*Kwanini unafanya mambo unayoyafanya na je, yanalingana na kiwango ulichonacho?

*Unautambuaje umuhimu wa watu katika maisha yako?

*Je? Ni vitu gani vinaweza kuchochea zaidi wito ulioko ndani yangu?

*Na je! Ni vitu gani vinaweza kusaidia kuharibu wito ulioko ndani yangu?

*Je nimejitoa kwa Mungu kwa jinsi anavyotaka? Kama sio, kwanini?

*Ninawafahamu adui wanaoweza kunizuia kufikia kilele cha maono niliyonayo?

*Nini nafasi ya marafiki katika kunisaidia kwenda mbele au kurudi nyuma katika safari yangu?

*Ninatambua nafasi ya wazazi na au walezi katika kukua kwangu kwa ujumla?

*Nikiwa peke yangu katika eneo la siri, huwa nawaza nini na vitu gani huwa nafanya kama mtumishi wa Mungu?

UMUHIMU WA KUJITAMBUA

*Ili kutembea au kuishi katika viwango asilia ambavyo umeumbwa navyo

Ili kujua madhaifu uliyonayo kwa ajili ya kujua namna ya kuyashinda
*Ili kujua thamani yako, uepuke kutumiwa vibaya, usijidharau wala kumtengenezea mtu mwingine mazingira ya kukudharau na hata usimdharau mtu mwingine

*Ili ujua nafasi yako (majukumu) katika maisha yako na ya wale wanaokuzunguka

*Ili kujua umuhimu ulionao kwa ajili ya kuleta matokeo yanayotarajiwa kwako

*Itakusaidia kutumia vizuri rasilimali kama muda, watu nk

MAHUSIANO KATI YA KUJITAMBUA NA MAENDELEO YA KIJANA

Kujitambua ni kuwa na ufahamu au uelewa juu ya :

qHistoria ya asili yako au maisha yako

qMaumbile yako,

qMakuzi na malezi yako,

qMazingira na jamii,

qHisia, utashi na ufahamu wako

qManeno na maamuzi yako,

qTabia na mwenendo

Au kwa lugha rahisi ni kuwa na ufahamu juu ya roho yako, nafsi yako na mwili wako katika maeneo yote ya kimaendeleo yaani kiroho, kimwili, kiakili na kijamii-hisia

*NAFASI YA NENO LA MUNGU

*Kujitambua nje ya Neno la Mungu kutakusaidia kuishi chini ya kiwango na ukiishi chini ya kiwango utapoteza thamani ya maisha yako kwa ujumla

*Neno la Mungu ndio lenye ukweli juu ya maisha yako yaliyopiata, maisha ya sasa na yale yajayo

*Linaitwa Neno la Mungu, lipe uzito na heshima yake ili uone matokeo yanayostahili

*Neno la Mungu linakujua wewe vizuri kuliko hata wazazi wako wanavyokufahamu, na ndio maana wengine wazazi wamewaabuse

*Weka mkakati wa kumjua Mungu kupitia neno lake, kumbuka, you cant give what you don’t have

*Kubali kulipa gharama kwani mabadiliko yanahitaji kulipa gharama yake

*Badilisha mfumo wako wa kufikiri kwanza, Waamuzi 6:1-16, Warumi 12:2

*Jifunze kuzitumia vizuri fursa unazozipata

*Chukua hatua ya maamuzi, 2 falme 7:3-19

*Badilisha aina ya vyakula unavyokula? Zaburi 19:14, Mathayo 12:33-36

*Fahamu umechaguliwa, Yohana 15:16

*Sifa za kuchaguliwa na Mungu, 1korintho 1:26-31

*Mfahamu wewe usiejulikana bado, 1korintho 2:6-10

*Badilisha maadui zako????? Mithali 18:24

*Ufanye nini kuanzia sasa? Mhubiri 12:1 na maombolezo 3:27

MATOKEO YA KUJITAMBUA

*Nidhamu

*Ujasiri

*Msimamo

*Kujiamini-confidence

*uwezo wa kufanya vitu kwa ubora-Competence

*Kuwa na mahusiano mazuri na watu wengine-Connection

*Kuwajali wengine

*Kujithamini

*Kuthubutu

*Mabadiliko ya tabia na mwenendo-character

*Kuwajibika

*Mabadiliko ya fikra
Maisha ni uchaguzi wako, unaweza kuamua utakavyo but usisahau kuwa kila maamuzi uyafanyayo utalipia gharama!

“Kiwango cha juu kabisa cha kujitambua ni kumjua Mungu kuwa ni wa pekee na wa kweli na kumjua mwanae wa pekee Yesu Kristo, kwa lugha nyingine kujitambua lazima kuanzie na kuishie na Yesu Kristo. Kujitambua nje ya Mungu ni ubatili mtupu, kujitambua nje ya Neno la Mungu ni kuigiza na kujitambau pasipo kumjua Mungu inaleta mahangaiko makubwa sana. Wengi wamejitambua kwa njia mbali mbali lakini bado kila siku wanazidi kuchoka kwa kuwa kujitambua lazima kukupe ahadi zenye umilele yaani kuurithi uzima wa milele”

“Transforming young generations for the glory of God and His Kingdom”